Show simple item record

dc.contributor.authorKemunto, Judith
dc.date.accessioned2016-04-21T14:09:50Z
dc.date.available2016-04-21T14:09:50Z
dc.date.issued2015
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/94681
dc.description.abstractKuna tafiti kadhaa zilizowahi kufanywa kuhusu majagina wa Kiafirika. Hata hivyo hakuna utafiti linganishi uliowahi kufanywa kuwahusu Fumo Liyongo na Sakawa. Tasnifu hii inazilinganisha sifa zao jinsi zinavyojitokeza katika Utenzi wa Fumo Liyongo (Kijumwa 1973) na Kivuli cha Sakawa (Matundura 2010) kwa kuzingatia nadharia ya uhakiki wa vikale. Historia yao pamoja na ya jamii wanamotoka mashujaa hawa zimechunguzwa ili kuweka msingi thabiti wa kuzichunguza sifa zao. Inadhihirika kwamba vikale hujitokeza katika vipindi na maeneo mbalimbali kwa kurejelea wakati na mazingira ambamo tungo hizi ziliandikwa. Isitoshe, vikale huwa havifungamanishwi na utanzu mmoja inavyobainika kutoka kazi hizi tulizozitumia katika utafiti huu. Kwa kuongozwa na ubia wa sifa za majagina utafiti umebainisha kwamba mashujaa hawa wana sifa kadha ambazo zinafanana kuliko zile zinazowatofautisha. Sifa zilizozingatiwa katika kuwalinganisha ni zile za kihistoria, kijamii na za kimaumbileen_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.subjectsifa za mashujaa, sakawa na fumo liyongoen_US
dc.titleUhakiki Linganishi Wa Sifa Za Mashujaa: Sakawa Na Fumo Liyongoen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record