Show simple item record

dc.contributor.authorNyandiwa, Hudson
dc.date.accessioned2016-04-22T07:35:14Z
dc.date.available2016-04-22T07:35:14Z
dc.date.issued2015
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/94804
dc.description.abstractUtafiti huu ulihusu uchanganuzi wa kimtindo katika Zinguo la Mzuka na Mbaya Wetu. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza matumizi ya sitiari, chuku, tashbihi, tashihisi, kejeli, tanakuzi na oksimora katika tamthilia zinazohusika. Tulichochewa na ufahamu kwamba mtindo na dhana ya maudhui ni vitengo muhimu vya fasihi ambavyo huandamana na kuegemeana ili kufanikisha dhamira ya mwandishi kwa wasomaji wa kazi yake. Uchochezi huu ulikuwa na ukweli kwamba matumizi ya tamathali za usemi huondoa uchapwa katika kazi za sanaa pamoja na kuwa matumizi ya tamathali za usemi si ya kiajali ila hutumika kimakusudi. Matumizi ya tamathali hizi huwa ni kuwasilisha ujumbe kimuktadha ili kuwezesha uelewa wa matini kwa kina. Utafiti uliongozwa na nadharia ya elimumitindo inayohusu uchanganuzi wa mbinu zote za lugha ambazo hutumika katika mawasiliano ambayo hujumuisha mawasiliano ya fasihi na mawasiliano yasiyokuwa ya fasihi. Ni wazi kuwa tamathali za usemi za sitiari, chuku, tashbihi, tashihisi, kejeli, tanakuzi na oksimora husheheni maana zinapotumika katika muktadha na bila muktadha ni vigumu kuchanganua tamathali yoyote kisemantiki. Kwa hivyo matini huzipa muktadha wa uchanganuzi. Baada ya kuzisoma tamthilia hizi tulitambua kuwa tamathali za usemi tulizotaja hapo juu zilitumika katika tamthilia za Mbaya Wetu na Zinguo la Mzuka. Tulizichanganua kwa kurejelea muktadha wa matumizi yazo kwenye matini hizi. Iligundulika kuwa matumizi ya vipengele vya tamathali za usemi vya sitiari, chuku, tashbihi, tashihisi, kejeli, tanakuzi na oksimora vimechangia katika kuibua, kuendeleza na kuwasilisha maudhui katika tamthilia zinazohusika. Kwa hivyo iligunduliwa kwamba msanii hutawala lugha kiufundi ili kuonyesha tofauti kati ya lugha ya fasihi na lugha ya kawaida. Aidha, tamathali za usemi hutumiwa na msanii kimakusudi. Kwa hivyo ujumbe ulioko kwenye tamathali hizi huwasilishwa kwa kuzingatia muktadha na vilevile, ni vigumu kuchanganua usemi wenye ukiushi ambao hutokea katika hali isiyokuwa na muktadha. Isitoshe, iligundiliwa kwamba ukiushi katika tamathali za usemi huwezesha uelewa wa kina wa matini. Muktadha wa kiisimu huchangia kutoa maana ambayo mwishowe huibua na kuwasilisha maudhui na kwa hivyo kuifanya kazi ya sanaa kuwa na maudhui ya pekee kutokana na ukiushi kwenye usemi huo na mwisho lugha huwa na uwili usioepukika, yaani uwakilishi wa maana ya kisanii na maana ya kimawasiliano. Napendekeza na kutilia mkazo kwamba vipengele vya fani kama vile muundo, wahusika na mandhari vichunguzwe katika tamthilia hizi mbili. Vilevile ukiushi wa kisintaksia, kileksika na wa kisarufi waweza kuchunguzwa. Aidha, nadharia tofauti na tuliyotumia yaweza kutumiwa.en_US
dc.language.isoOtheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleUchanganuzi Wa Kimtindo Wa Zinguo La Mzuka Na Mbaya Wetuen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record