Familia za kiafrika katika njia panda: mitagusano na, changamano za usasa katika mhanga nafsi yangu
View/ Open
Date
2015Author
S.A Mohamed, Jackline Munyoki
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Naungama kuwa kazi hii haikuwa rahisi kuitekeleza lakini kupitia kwa wasimamizi wangu
nimeweza kufaulu. Kujitolea kwao ni zaidi ya ilivyotarajiwa maana hawakuchoka kusoma kwa
kina kazi hiyo na kunielekeza ipasavyo. Shukrani za dhati ni kwa Dkt. Omboga Zaja na Dkt.
Amiri Swaleh waliyojitolea mhanga kuona kazi niliyokuwa nikiishughulikia imeafikiana
kulingana na matarajio ya kozi. Urekebishaji na uelekezaji wao ulikuwa wa wazi na wa kufaa
mno maaana nilipoirejelea kazi yenyewe, niliweza kuona niliyostahili kutekeleza. Nawapa
kongole kwa vile waliweza kunishauri na kunielekeza ipasavyo kwani ushauri wao ulinipa nguvu
na maarifa ya kushughulikia kazi yangu. Yakini usimamizi wao ulinifaa zaidi na ndiyo maana
nimefaulu katika tasnifu yangu.Aidha nawashukuru wafuatao: Dkt. Iribe, Profesa Habwe na
Profesa Kineene kwa maoni yao ya kutia moyo na kujitolea kwao nilipowahitaji. Ombi langu ni
Rabuka awabariki kwa kazi zao nzuri.Tena sitawasahau wanakufunzi wenzangu ambao kwa
pamoja tuliweza kushirikiana katika masomo ya uzamili kupitia kazi ya vikundi na mijadala
tuliyojihusisha nayo kwa lengo la kudurusu kozi zetu. Ushauri wao wa kutia moyo ulinipa motisha na nguvu ya kuendelea.