Maudhui ya uadilifu katika nyimbo za Joseph Ngala
View/ Open
Date
2015Author
Kanyange, Evaline K.
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulikia maudhui ya uadilifu katika nyimbo tulizoteua tisa za Joseph Ngala
ambazo ni Fuateni mambo ya sheria, Mwana Mpotevu, Ndivyo Ilivyo dunia, Nisikilize
Mwanangu, Ndugu Tupendane, Dada Vumilia, Simba, Kisulisuli na Jembe. Tulilenga kubainisha
matendo adilifu yanayojitokeza katika nyimbo hizi, kutoa sababu thabiti za kuainisha matendo
hayo kama adilifu kwa kutumia nadharia ya unufaishaji hasi kisha tulieleza matendo hayo
yanatoa athari zipi kwa walengwa ambao ni jamii/ mtu binafsi. Matokeo ya utafiti wetu
yalidhihirisha bayana kuwa msanii Joseph Ngala ameangazia pakubwa maudhui ya uadilifu
katika nyimbo zake ambayo ni pamoja na kutii sheria, kutokuwa na tamaa, kusikiliza mawaidha
kutoka kwa wakuu, upendo, uvumilivu, shukrani, ushirikiano na uwajibikaji. Aidha, tulibainisha
kuwa matendo haya yanatoa athari chanya kwa jamii/ mtu binafsi.
Publisher
University of Nairobi