Show simple item record

dc.contributor.authorSito, Paul S
dc.date.accessioned2016-04-28T06:09:44Z
dc.date.available2016-04-28T06:09:44Z
dc.date.issued2015
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/95196
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu athari za mazingira katika uteuzi wa msamiati. Tumetumia methali za Kiswahili zinazorejelea viumbe wa majini kama data ya uchanganuzi wetu. Utafiti huu una jumla ya sura tano. Tatizo letu la utafiti limetokana na ukweli kwamba hakuna maana moja inayojitokeza ili kueleza dhana ya methali. Wataalamu mbalimbali wamefafanua dhana ya methali kwa mujibu wa mkabala ambao wanaufasili. Ndiposa utafiti wetu umezamia suala la mazingira na mchango wake katika uteuzi wa msamiati katika methali za Kiswahili zinazorejelea viumbe wa majini, msamiati ulioteuliwa hukusudiwa kuafikia malengo gani kwa jamii na jinsi msamiati ulioteuliwa unatusaidia kuelewa mahusiano na maafikiano ya watu katika jamii inayotumia lugha ya Kiswahili. Utafiti wetu una madhumuni matatu: kufafanua sifa, tabia na maumbile ya viumbe walioteuliwa na kutumiwa katika methali za Kiswahili zinazorejelea viumbe wa majini, kueleza athari zinazotokana na matumizi ya methali za Kiswahili zinazorejelea viumbe wa majini katika jamii ambamo lugha ya Kiswahili hutumiwa, kuchunguza uamilifu wa methali za Kiswahili zinazorejelea viumbe wa majini katika mazingira mahsusi. Madhumuni yetu yametokana na nadharia tete zetu kuwa kunao viumbe wenye maumbile, sifa, na tabia mahsusi ambao kwa mujibu wa wanajamii hutumika katika methali za Kiswahili, na kwamba maumbile, sifa na tabia za viumbe hao zinafaa kwa matumizi ya methali mahsusi katika jamii ya Waswahili, athari zinazotokana na matumizi ya msamiati wa Kiswahili unaohusu methali za Kiswahili zinazorejelea viumbe wa majini zinaonekana na kwamba methali za Kiswahili zinazorejelea viumbe wa majini huwa na uamilifu fulani katika utekelezaji wa majukumu fulani katika mazingira mahsusi. Utafiti wetu umeongozwa na nadharia ya mahusiano, ambapo dhana zake tatu za utambuzi, mawasiliano na uelewa zimetuongoza katika utafiti huu. Katika utafiti wetu tumetoa maelezo kuhusu dhana muhimu katika utafiti huu, na pia kuangazia methali kwa ujumla wake. Pia tumefanya ufafanuzi wa methali za Kiswahili zinazorejelea viumbe wa majini kwa kuangazia sifa, tabia na maumbile ya viumbe waliotumika katika methali hizo. Katika uchanganuzi wa data, utafiti wetu umethibitisha kuwa mazingira ni muhimu sana katika uteuzi wa msamiati. Msamiati ulioteuliwa na kutumika katika methali husika huwa na athari kwa wanajamii na kuwa methali hizo husika huwa na uamilifu wa majukumu katika jamii.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleAthari za mazingira katika uteuzi wa msamiati: mfano wa methali za kiswahili zinazorejelea viumbe wa majinien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record