Show simple item record

dc.contributor.authorKiongera, J Kiarie
dc.date.accessioned2013-02-12T14:48:06Z
dc.date.available2013-02-12T14:48:06Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/9546
dc.description.abstractKazi hii inahusu juhudi za vijana kama mawakala wa mabadiliko chanya katika tamthilia nne za Kiswahili. Tamthilia hizi ni Kifo Kisimani naMaua Kwenye Jua la Asubuhi zilizoandikwa na Kithaka wa Mberia . Pango na Seserumbe, zilizoandikwa na K W. Wamitila ,Tumeongozwa na nadharia ya Ki-Foucault iliyoasisiwa na Micheal Foucault. Huyu ni mwananadharia wa Kifaransa aliyeishi baina ya mwaka wa 1926 hadi 1984. Tunaangazia mtazamo wake kuhusu mahusiano ya mamlaka na upinzani unaozuka pale panapokiukwa maadili ya mahusiano yenyewe. Upinzani tunaouchanganua ni ule unaoongozwa na wahusika vijana katika tamthilia nne tulizoziteua Katika sura ya kwanza, tumechunguza maswala ya kimsingi yanayodhamiria kujenga msingi wa utafiti wetu kama vile: Sababu za kushughulikia mada, tatizo la utafiti, yaliyoandikwa kuhusu vijana, upeo na mipaka ya utafiti. Tumeongozwa na nadharia tete zifuatazo: kwamba vijana wamefanikiwa kuyaleta mabadiliko na kwamba wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katikajitihada zao. Katika sura ya pili tumeijadili dhana ya vijana na kuyachunguza maovu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hapo tumewaonyesha vijana wakikabiliana na maovu hayo ili kuleta mabadiliko chanya. Katika sura ya tatu tumechunguza mafanikio waliyoyapata vijana katika kuzibadilisha jamii zao. Pia tumechunguza changamoto zinazowakabili katika harakati zao za kuleta mabadiliko chanya Katika sura ya nne tumetoa muhtasari wa utafiti rnzima na mapendekezo ya tafiti zaidi zinazoweza kufanywa kuhusiana na mada yetu.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleMchango wa vijana kuleta mabadiliko chanya katika tamthilia teule za Kiswahilien_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record