Maudhui Ya Ukombozi Katika Wimbo Mpya Na Msururu Wa Usaliti
Abstract
Tasnifu hii imeshughulikia swala la Maudhui ya Ukombozi katika Wimbo Mpya na Msururu wa
Usaliti. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kutathmini changamoto zinazozikumba jamii za
Wimbo Mpya na Msururu wa usaliti, kuchunguza aina tofauti za ukombozi katika riwaya hizi
mbili na pia kuonyesha mikakati ya kujikomboa wanayoitumia wanajamii wa Wimbo Mpya na
Msururu wa Usaliti. Utafii huu uliongozwa na nadharia ya U- Marx. Nadharia hii iliasisiwa na
Karl Marx na Friedrich Engels kati ya miaka ya 1818 na 1895. Hii ni nadharia ya kiukombozi
inayoeleza namna migogoro ya kitabaka hupelekea tabaka la chini kujikomboa kutokana na
mfumo wa kibepari unaoendelezwa na tabaka la juu dhidi ya tabaka hili. Utafiti huu uligundua
kwamba riwaya za Wimbo Mpya na Msururu wa Usaliti zimefaulu katika kuonyesha chanzo cha
vita vya ukombozi katika jamii zote mbili. Riwaya hizi zimebainisha kuwa chanzo cha vita vya
ukombozi katika jamii hizi kilikuwa ni changamoto zilizowakumba wanajamii hawa.
Changamoto zenyewe ni ukoloni, ukosefu wa elimu, utabaka, mvutano baina ya usasa na ukale,
dhuluma dhidi ya wanawake, uharibifu wa mazingira, ufisadi, uongozi mbaya na umaskini.
Vilevile, utafiti huu ulibainisha kuwa jamii za Wimbo Mpya na Msururu wa Usaliti
zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika juhudi zao za ukombozi wa aina tofautitofauti kwa
kuwa walibuni mikakati ifaayo ya kujikomboa. Ukombozi waliouendeleza wanajamii hawa ni
ukombozi unaolenga maswala anuai yanayomzingira mwanadamu yakiwemo ya kiuchumi,
kijamii na kisiasa.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: