Show simple item record

dc.contributor.authorKimeu, Adeline N
dc.date.accessioned2016-11-14T12:23:11Z
dc.date.available2016-11-14T12:23:11Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/97138
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia swala la Maudhui ya Ukombozi katika Wimbo Mpya na Msururu wa Usaliti. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kutathmini changamoto zinazozikumba jamii za Wimbo Mpya na Msururu wa usaliti, kuchunguza aina tofauti za ukombozi katika riwaya hizi mbili na pia kuonyesha mikakati ya kujikomboa wanayoitumia wanajamii wa Wimbo Mpya na Msururu wa Usaliti. Utafii huu uliongozwa na nadharia ya U- Marx. Nadharia hii iliasisiwa na Karl Marx na Friedrich Engels kati ya miaka ya 1818 na 1895. Hii ni nadharia ya kiukombozi inayoeleza namna migogoro ya kitabaka hupelekea tabaka la chini kujikomboa kutokana na mfumo wa kibepari unaoendelezwa na tabaka la juu dhidi ya tabaka hili. Utafiti huu uligundua kwamba riwaya za Wimbo Mpya na Msururu wa Usaliti zimefaulu katika kuonyesha chanzo cha vita vya ukombozi katika jamii zote mbili. Riwaya hizi zimebainisha kuwa chanzo cha vita vya ukombozi katika jamii hizi kilikuwa ni changamoto zilizowakumba wanajamii hawa. Changamoto zenyewe ni ukoloni, ukosefu wa elimu, utabaka, mvutano baina ya usasa na ukale, dhuluma dhidi ya wanawake, uharibifu wa mazingira, ufisadi, uongozi mbaya na umaskini. Vilevile, utafiti huu ulibainisha kuwa jamii za Wimbo Mpya na Msururu wa Usaliti zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika juhudi zao za ukombozi wa aina tofautitofauti kwa kuwa walibuni mikakati ifaayo ya kujikomboa. Ukombozi waliouendeleza wanajamii hawa ni ukombozi unaolenga maswala anuai yanayomzingira mwanadamu yakiwemo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMaudhui Ya Ukombozi Katika Wimbo Mpya Na Msururu Wa Usalitien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States