Show simple item record

dc.contributor.authorAdicka, Polycap O
dc.date.accessioned2016-11-21T11:33:11Z
dc.date.available2016-11-21T11:33:11Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/97633
dc.description.abstractUtafiti huu ni uchunguzi wa utohozi wa nomino za lahaja ya Kijaluo ya Nyanza Kusini ambazo zimetoholewa kutokana na lugha ya Kiswahili. Nomino hizi za mkopo zimechanganuliwa ili kutathmini michakato ya kiutohozi inayotumiwa kwenye harakati za ukopaji wa maneno hayo (ya Kijaluo) kutoka lugha ya Kiswahili. Michakato hiyo inaangaziwa katika viwango viwili vya kiisimu: kiwango cha kifonolojia na kile cha mofolojia. Uchanganuzi huu unaongozwa na mkabala wa mlingano-chanzi ambao ni kimelea cha nadharia ya upeo. Nadharia hii inashikilia kuwa maumbo ya maneno-mkopo yanatokana na mtagusano baina ya kanuni zinazokinzana za lugha husika. Miongoni mwa kanuni hizo ni kanuni ya uaminifu ambao unasisitiza ulinganifu katika miundo ya nje ya vipande-sauti vya lugha-changizi na vile vya lugha-pokezi. Kanuni hii ndiyo uti wa mgongo wa mkabala wa mlingano-chanzi. Mkabala huu unafafanua mifanano iliyopo katika maumbo ya vipande sauti vya lugha-pokezi (Kijaluo) na vile vya lugha-changizi (Kiswahili). Matokeo yameonyesha kuwa ingawa mfanyiko wa utohozi huongozwa na mikakati mbalimbali ya kifonolojia na kimofolojia, kuna mfanano mkubwa kati ya lugha-pokezi na lugha-changizi. Hali hii inaelezeka kwenye mtazamo wa mlingano-chanzi kupitia kanuni yake ya uaminifu. Kifonolojia, taratibu za kiutohozi zilizobainishwa ni: udondoshaji, uchopekaji na ubadilishaji-sifa. Kwa upande mofolojia, utaratibu wa kiutohozi uliotamalaki kwenye utohozi wa maneno ya Kiswahili yanayoingia katika Kijaluo ni uambishaji.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectMtazamo Wa Mlingano Chanzien_US
dc.titleUtohozi Wa Wa Maneno-mkopo Katika Lugha Ya Kijaluo Kutoka Kiswahili: Mtazamo Wa Mlingano Chanzien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States