dc.description.abstract | Tamthilia ya Kiswahili ni mojawapo ya tanzu za Fasihi Andishi ya Kiswahili. Tanzu nyingine ni pamoja na riwaya, ushairi, hadithi fupi, novela na zinginezo. Utanzu wa tamthilia umedhihirisha kwa njia moja au nyingine uhusiano wa kimwingilianomatini. Utafiti huu umelenga kuchunguza na kuchanganua mwingilianomatini kati ya tamthilia za Mstahiki Meya (Arege,2009) na Mkaguzi Mkuu wa serikali (Gogol,1979). Katika kuhakiki hayo, tumetumia nadharia ya Mwingilianomatini iliyoasisiwa na mwana nadharia wa Kifaransa Julia Kristeva. Tumeongozwa na malengo matatu ya utafiti-kuchunguza jinsi tamthilia zinavyoingiliana kifani na kimaudhui vilevile kuchunguza iwapo nadharia ya Mwingilianomatini inafaa katika uhakiki wa tamthilia ya Kiswahili. Utafiti umeongozwa na maswali yafuatayo: Je, tamthilia hizi zina mwingiliano au la, zikiwa zinao, basi kwa kiwango gani? Je, ni sehemu zipi za tamthilia zinaingiliana kwa mujibu wa mwanda wa mwingilianomatini? Kutokana na utafiti huu, imebainika wazi kwamba tamthilia ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Mstahiki Meya zinaingiliana katika vipengele vya msuko, usawiri wa wahusika, mandhari na maudhui. Maswali yetu ya utafiti yamepata kujibiwa kikamilifu kwa kuwa tumeweza kuonyesha jinsi tamthilia zinavyoingiliana na kuchangizana. Hatimaye, tumetoa mapendekezo kwa watakaofanya tafiti za baadaye kuhusiana na swala la kuingiliana kwa matini. | en_US |