Show simple item record

dc.contributor.authorNyamari Roseline K
dc.date.accessioned2016-11-23T10:19:54Z
dc.date.available2016-11-23T10:19:54Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/97773
dc.description.abstractUtafiti huu umehusu namna ambavyo mtindo umetumika katika Utenzi wa Katirifu mswada wa Knappert (1979). Tumehakiki vipengele vya kimtindo ambavyo ni wahusika, taswira, dayalojia na tamathali nyingine za usemi zikiwemo maswali ya balagha, tashihisi, tashibihi, chuku na sitiari. Katika kuhakiki hayo, tumeitumia nadharia ya Umitindo. Tumeongozwa na malengo mawili ya utafiti. Kwanza, kuhakiki vipengele vya kimtindo katika Utenzi wa Katirifuna pili, kubainisha umuhimu wa vipengele hivyo katika kuwasilisha dhamira na maudhui ya mtunzi. Kuhusu wahusika, tumehakiki sifa zinazowatambulisha na uhusika wao katika Utenzi wa Katirifu. Wahusika wasaidizi wamewasaidia wahusika wakuu katika kujenga na kukamilisha maudhui ya mwandishi. Taswira, dayalojia na tamathali za usemi zimetumiwa kuwasilisha dhamira na maudhui yake. Kuna mandhari ya kijiografia na yale ya kinjozi. Maswali yetu ya utafiti yamepata kujibiwa kikamilifu kwa kuwa tumeweza kubaini vipengele vya kimtindo na pia kuonyesha umuhimu wa vipengele hivyo katika uwasilishaji wa dhamira na maudhui. Hatahivyo, kuna changamoto tulizozipitia. Hatimaye, tumetoa mapendekezo kwa watakaofanya tafiti za baadaye kuhusiana na Utenzi wa Katirifu.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity Of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMtindo Katika Utenzi Wa Katirifu.en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States