Mielekeo Ya Jamiilugha Ya Kimaasai Kuhusu Kiswahili
View/ Open
Date
2016Author
Kaindi, Gladys N
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Katika tasnifu hii, tumechunguza mielekeo ya jamiilugha ya Kimaasai kuhusu Kiswahili.
Utafiti wenyewe umejikita katika kuchunguza masiala yanayosababisha lugha ya Kiswahili
ambayo ni rasmi Kenya kutotumika katika diskosi rasmi katika tarafa ya Kitengela wilayani
Isinya kaunti ya Kajiado. Mbinu tulizotumia ni hojaji za kujazwa na mahojiano ya moja kwa
moja.Tuliweza kutumia maswali ya wazi, maswali funge na maswali ya viwango.
Waliopendelea lugha yao ya asili katika kujaza hojaji walipewa maswali yaliyokuwa katika
lugha ya Kimaasai.Viongozi mbalimbali pamoja na wakazi wa umri mkubwa na mdogo
wenye asili ya Kimaasai ndio waliohusishwa katika mahojiano pamoja na kujaza hojaji.
Data ilichanganuliwa kwa kutumia baa grafu,majedwali ya frikwenzi pamoja na pai chati.
Nadharia jumuishi na utambulisho ya Giles (1979) ndio iliyotumika. Matokeo ya utafiti
yalikuwa kwamba jamiilugha ya Kimaasai katika tarafa ya Kitengela ina mielekeo hasi na
chanya kuhusu lugha ya Kiswahili kwa kutegemea viathiriwa vilivyotumiwa.Watafitiwa
walio na umri mkubwa walithamini lugha ya Kimaasai ikiwa ni lugha ya jadi kwa
madhumuni ya kudumisha utamaduni , imani, mila na desturi. Walio na umri mdogo
wanaendelea kupoteza umilisi wao wa lugha asili kutokana na hali ya mabadiliko ya maisha
ya jamii ya Wamaasai kadri miaka zinavyozidi kupita. Mapendekezo yalikuwa, kwa kuwa
lugha ya Kiswahili ni rasmi viongozi watumie katika mikutano rasmi kwani ndio lugha
inayoweza kuleta hisia za undugu na mshikamano miongoni mwa jamiilugha mbalimbali.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: