Show simple item record

dc.contributor.authorKaindi, Gladys N
dc.date.accessioned2017-01-04T05:42:47Z
dc.date.available2017-01-04T05:42:47Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/98651
dc.description.abstractKatika tasnifu hii, tumechunguza mielekeo ya jamiilugha ya Kimaasai kuhusu Kiswahili. Utafiti wenyewe umejikita katika kuchunguza masiala yanayosababisha lugha ya Kiswahili ambayo ni rasmi Kenya kutotumika katika diskosi rasmi katika tarafa ya Kitengela wilayani Isinya kaunti ya Kajiado. Mbinu tulizotumia ni hojaji za kujazwa na mahojiano ya moja kwa moja.Tuliweza kutumia maswali ya wazi, maswali funge na maswali ya viwango. Waliopendelea lugha yao ya asili katika kujaza hojaji walipewa maswali yaliyokuwa katika lugha ya Kimaasai.Viongozi mbalimbali pamoja na wakazi wa umri mkubwa na mdogo wenye asili ya Kimaasai ndio waliohusishwa katika mahojiano pamoja na kujaza hojaji. Data ilichanganuliwa kwa kutumia baa grafu,majedwali ya frikwenzi pamoja na pai chati. Nadharia jumuishi na utambulisho ya Giles (1979) ndio iliyotumika. Matokeo ya utafiti yalikuwa kwamba jamiilugha ya Kimaasai katika tarafa ya Kitengela ina mielekeo hasi na chanya kuhusu lugha ya Kiswahili kwa kutegemea viathiriwa vilivyotumiwa.Watafitiwa walio na umri mkubwa walithamini lugha ya Kimaasai ikiwa ni lugha ya jadi kwa madhumuni ya kudumisha utamaduni , imani, mila na desturi. Walio na umri mdogo wanaendelea kupoteza umilisi wao wa lugha asili kutokana na hali ya mabadiliko ya maisha ya jamii ya Wamaasai kadri miaka zinavyozidi kupita. Mapendekezo yalikuwa, kwa kuwa lugha ya Kiswahili ni rasmi viongozi watumie katika mikutano rasmi kwani ndio lugha inayoweza kuleta hisia za undugu na mshikamano miongoni mwa jamiilugha mbalimbali.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMielekeo Ya Jamiilugha Ya Kimaasai Kuhusu Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States