Uchambuzi Linganishi Wa Fani Na Maudhui Ya Nyimbo Za Harusi Za Kimeru Na Za Kiswahili
View/ Open
Date
2017Author
Gitonga, Norah, W
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulikia uchambuzi linganishi wa fani na maudhui katika nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili. Tumerejelea nadharia mbili, ambazo ni nadharia ya uhalisia na umitindo. Nadharia ya uhalisia imetusaidia katika ufafanuzi wa maudhui, nao mtazamo wa umitindo wa Leech (1969) imetusaidia kubainisha vipengele vya fani ambavyo msanii ametumia ili kuwasilisha ujumbe wake kwa hadhira. Lengo letu ni kulinganisha na kutofautisha maudhui na fani katika nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili. Tumefanya hivi kwa kukusanya baadhi ya nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili, na hatimaye kuzichambua. Tumezipata nyimbo hizo kwa kufanya utafiti wa nyanjani kwa kuhudhuria sherehe za harusi, kuwahoji watu wenye tajriba katika nyimbo hizo na pia kwa kutumia mitandao. Nadharia tete ambazo tumetumia ni kutaka kuthibitisha iwapo kuna uhusiano na tofauti za kimaudhui na kifani katika nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili. Utafiti wetu umetuwezesha kuthibitisha kuwa kuna baadhi ya maudhui ambayo yanalingana katika nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili. Vile vile tumeweza kuthibitisha kuwa kuna fani zinazolingana na pia kutofautiana katika nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili. Katika kuhitimisha utafiti wetu, tumegusia changamoto tulizokumbana nazo na tukatoa mapendekezo ambayo yanaweza kuwafaa watafiti wa hapo baadaye.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Education (FEd) [5964]
The following license files are associated with this item: