Show simple item record

dc.contributor.authorGitonga, Norah, W
dc.date.accessioned2017-12-08T12:51:02Z
dc.date.available2017-12-08T12:51:02Z
dc.date.issued2017
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/101711
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia uchambuzi linganishi wa fani na maudhui katika nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili. Tumerejelea nadharia mbili, ambazo ni nadharia ya uhalisia na umitindo. Nadharia ya uhalisia imetusaidia katika ufafanuzi wa maudhui, nao mtazamo wa umitindo wa Leech (1969) imetusaidia kubainisha vipengele vya fani ambavyo msanii ametumia ili kuwasilisha ujumbe wake kwa hadhira. Lengo letu ni kulinganisha na kutofautisha maudhui na fani katika nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili. Tumefanya hivi kwa kukusanya baadhi ya nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili, na hatimaye kuzichambua. Tumezipata nyimbo hizo kwa kufanya utafiti wa nyanjani kwa kuhudhuria sherehe za harusi, kuwahoji watu wenye tajriba katika nyimbo hizo na pia kwa kutumia mitandao. Nadharia tete ambazo tumetumia ni kutaka kuthibitisha iwapo kuna uhusiano na tofauti za kimaudhui na kifani katika nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili. Utafiti wetu umetuwezesha kuthibitisha kuwa kuna baadhi ya maudhui ambayo yanalingana katika nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili. Vile vile tumeweza kuthibitisha kuwa kuna fani zinazolingana na pia kutofautiana katika nyimbo za harusi za Kimeru na za Kiswahili. Katika kuhitimisha utafiti wetu, tumegusia changamoto tulizokumbana nazo na tukatoa mapendekezo ambayo yanaweza kuwafaa watafiti wa hapo baadaye.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUchambuzi Linganishi Wa Fani Na Maudhui Ya Nyimbo Za Harusi Za Kimeru Na Za Kiswahilien_US
dc.titleUchambuzi Linganishi Wa Fani Na Maudhui Ya Nyimbo Za Harusi Za Kimeru Na Za Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States