Mwingilianomatini Katika Utenzi Wa Fumo Liyongo Na Tamthilia Ya Kifo Kisimani
View/ Open
Date
2019Author
Kilingo, Irene G
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Matini huweza kuakisiana kwa namna moja ama nyingine. Sababu ni kwamba, waandishi hujihusisha na kukusanya na kupanga yaliyoko katika kazi za awali ili kuunda kazi zao. Kwa sababu hii, kazi itakayoundwa itakuwa na mshabaha fulani wa kazi nyingine ya awali. Matini za kifasihi zinaweza kuingiliana kimatini. Mwingiliano huu unaweza kubainika sio tu katika kazi za utanzu mmoja bali pia katika kazi za tanzu tofauti za kifasihi. Utafiti huu umelenga kuthibitisha kauli hii kwa kuchunguza mwingilianomatini katika Utenzi wa Fumo Liyongo na tamthilia ya Kifo Kisimani. Katika kuhakiki haya, tumetumia nadharia ya mwingilianomatini iliyoasisiwa na mwananadharia wa Kifaransa; Julia Kristeva. Kutokana na utafiti huu, imebainika kuwa, kuna kuna vipengele vya mwingilianomatini katika Utenzi wa Fumo Liyongo na Kifo Kisimani. Hali kadhalika, kazi hizi zimeonyesha kuingiliana katika viwango vya usimulizi, maudhui, dhamira, uhusika na pia mandhari. Aidha, athari za mwingilianomatini katika udhamirishaji na mtindo wa tamthilia ya Kifo Kisimani zilibainika. Utafiti huu umethibitisha kuwa kuna mwingilianomatini katika Utenzi wa Fumo Liyongo na Kifo Kisimani.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: