Jumbe Katika Leso: Matumizi Va Mbinu Va Kusutalf
Abstract
Katika utafiti huu tunalenga kuchanganua jumbe za kusuta katika leso mjini Mombasa
tukiongozwa na nadharia ya Upole. Utafiti huu ulihusu jumbe za kusuta za leso mjini
Mombasa. Utafiti huu ulikuwa unachunguza haipothesia nne kwamba a) maudhui ya
kusuta, umbeya na mapenzi yanatawala katika leso mjini Mombasa, b) Lugha ya
kitamathali hujitokeza katika mbinu ya kusuta katika kuwasilisha jumbe za Ieso, c)
Lugha sanifu ndiyo lugha inayopendelewa katika maandishi ya leso mjini Mombasa
na d) Kuna mitindo tofauti ya lugha inayotumika katika leso mjini Mombasa. Data
ilikusanywa kutoka maduka makuu ya leso mjini Mombasa. Kutokana na data hii,
sampuli ya jumbe 100 ilichaguliwa ili kuchanganuliwa. Data ilichanganuliwa kwa
kutumia majedwali na vielelezo vya nambari na maelezo ya matokeo kujadiliwa.
Utafiti huu umegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti na
katika sura ya pili tumejadili kwa kina suala zima la leso. Katika sura ya tatu
tumeainisha maudhui na sura ya nne tukaainisha mitindo ya lugha iliyotumika katika
jumbe za kusuta za leso. Mwishowe tukatoa muhtasari, hitimisho, changamoto za
utafiti, mapendekezo na matokeo ya utafiti katika sura ya tano.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [607]
The following license files are associated with this item: