Athari Za Udhanaishi Katika Kichwamaji Na Nguvu Ya Sala
View/ Open
Date
2006Author
Ngonge, Lilian G
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imechunguza athari za udhanaishi katika riwaya mbili ambazo ni Kichwamaji na
Nguvu ya Sa/a. Kazi yenyewe imegawika katika sura nne.
Katika sura ya kwanza tumetanguliza kwa ufupi dhana ya udhanaishi. Vilevile, tumebainisha
tatizo linalotafitiwa, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchagua mada, pamoja na
njia za utafiti. Aidha tumeangazia udurusu wa kazi mbalimbali pamoja na msingi wa kinadharia.
Tumetumia nadharia ya kisosholojia inayosisitiza umuhimu wa mazingira yaliyoibusha kazi ya
msanii.
Katika sura ya pili, tumeonyesha athari za udhanaishi zinazobainika katika riwaya ya
Kichwamaji. Vilevile mazingira mbalimbali ambayo yamemwathiri Kezilahabi na kumfanya
achukue mtazamo wa kidhanaishi yamejadiliwa.
Sura ya tatu imeangazia udhanaishi katika Nguvu ya Sa/a. Tumebainisha athari za udhanaishi
kupitia maudhui mbalimbali. Aidha tumeonyesha vile ambavyo mwandishi ameathiriwa na
mazingira alimoandikia.
Sura ya nne ni hitimisho. Tumehitimisha kwa kutoa maom kuhusiana na kazi hii kwa
ujumla. Vilevile, tumetoa mapendekezo ya utafiti zaidi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [606]
The following license files are associated with this item: