Matumizi Ya Taswira Kama Klgezo Cha Kufanikisha Maudhui Katlka Utendi Wa Siiraji Uliyotungwa Na Muhammad I Kijumwa
View/ Open
Date
2012Author
Ngunjiri, Dadson M
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Somo letu la utafiti linashughulikia matumizi ya taswira kama kigezo cha kufanikisha
maudhui katika Utendi wa Siiraji.
Utafiti wetu unanuia kuchunguza kigezo cha taswira na umuhimu wake katika
kufanya maudhui ya mtunzi yawe ya kutambuliwa na kuthaminika na msomi .
Kwenye sura ya kwanza tumechunguza masuala; Mwanzo tumetanguliza kuhusu
mada tunayoshughulikia, tatizo la utafiti, nadharia tete, umuhimu wa kushughulikia
mada, upeo na mipaka, yaliondikwa kuhusu Utendi wa Siiraji, msingi wa nadharia na
njia ya utafiti. Taswira tunayoishughulikia ni taswira chanya inayofungamanishwa na
maudhui ya utendi tunaouhakiki.
Sura ya pili inahusu historia ya mwandishi. Sura hii inatoa maisha ya mtunzi,
Muhammadi Kijumwa kwenye daraja zifuatazo; asili yake, elimu, ndoa yake, ndoa
ya Kiislamu, Ndoa ya Kikristo, asasi halisi ya mtunzi, mchango wake kwenye uwanja
wa fasihi, kazi alizozitunga, kazi alizozinakili, kazi alizotafsiri, nyimbo alizotunga,
tutumbi na barua alizoandika, uhusiano wake na wageni na pia wenyeji, dini na imani
ya mtunzi.
Sura ya tatu imeshughulikia dhana ya talaka kwa mjibu wa dini ya Kikristo, Kiislamu,
dhana ya maadili kwenye tungo za kishairi, na dhana ya taswira.
Sura ya nne ndiyo upeo wa utafiti wetu kwani inashughulikia asili ya Utendi wa
Siiraji, dhana ya maudhui kwenye utendi na jinsi kigezo cha taswira kimeunganishwa
na maudhui. Maudhui makuu yanayojitokeza kwenye utendi kama vile; ushirikiano,
ukarimu, tabia njema, usiri, suluhisho na mapatano, asasi ya ndoa, bidii, wema na utu,
Mwisho ni sura ya tano, ambayo inasheheni hitimisho la kazi nzima na mapendekezo
kuhusu uhakiki uliyo shughulikiwa. Ni sura hii ambayo imependekeza kazi kadhaa ya
utafiti wa ziada.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [607]
The following license files are associated with this item: