Urudiaji Na Uwasilishaji Wa Maana Katika Ushairi Wa Kisasa
Abstract
Tasnifuhii imeshughulikia urudiaji na uwasilishaji wa maana katika diwani ya Dhifa na Vifaru
Weusi. Tumeangazia mambo yafuatayo: usuli, suala la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya
utafiti,sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada,
msingiwa kinadharia na mbinu tulizotumia kufanya utafiti. Tumeeleza aina mbalimbali za
urudiajikama sehemu ya kimsingi ya ubainishaji wa viwango vya urudiaji. Tumetoa maana za
ainaza urudiaji na kuzigawa katika vitengo vitatu vikuu ambavyo ni: urudiaji sahili, urudiaji wa
kimaumbona urudiaji wa kimuundo. Tumechunguza aina za urudiaji kama zinavyojitokeza
katikadiwani ya Dhifa na Vifaru Weusi kwa kutoa mifano mwafaka ili kudhihirisha namna
ambavyowashairi wametumia urudiaji kuwasilisha maana na kuendeleza dhamira. Tumeangazia
dhimana athari ya urudiaji kama mbinu ya kipekee inayotumiwa na washairi kuwasilisha maana
na kuthibitisha namna urudiaji unavyomwathiri mpokeaji kwa kuelezea dhima zifuatazo:
usisitizajiwa maana, uelewekaji, upigaji mwangwi, suala la wizani, ukumbukaji, suala la ujumi
nauziada.Tumehitimisha kwa kutoa muhtasari wa utafiti na mapendekezo ya tafiti nyinginezo.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [638]
The following license files are associated with this item: