Muundo Na Uamilifu Wa Chagizo Katika Viral Na Vishazi Vya Kisw Ahili Sanifu
View/ Open
Date
2019Author
Mutai, Grace Wairimu
Type
ThesisLanguage
enMetadata
Show full item recordAbstract
Mada yetu ya utafiti ilikuwa uamilifu wa chagizo katika virai na vishazi vya Kiswahili
sanifu.Tulidhamiria kuchunguza viambajengo vya aina tofauti za chagizo katika virai na vishazi
vya Kiswahili sanifu huku tukilenga kuonyesha miundo ~i inayowakilishwa na aina hizi za
chagizo. Tulikusudia kubaini iwapo chagizo zenye miundo fulani huwakilisha majukumu yale
yale ya theta au tofauti iwapo nafasi ya chagizo husika itabadilishwa katika sentensi fulani. Utafiti
wetu ulitumia nadharia ya X-baa na Theta. Nadharia ya X-baa ilitumika kubainisha miundo tofauti
inayowakilishwa na chagizo katika virai na vishazi vya Kiswahili sanifu na ile ya Theta ilitumiwa
kutambua majukumu tofauti ya theta yanayowakilishwa na chagizo hizi katika virai na vishazi vya
Kiswahili sanifu.Data iliyotumika katika utafiti wetu ilidondolewa kutoka kwa vitabu vitatu tofauti
ambavyo vilihusisha sentensi zilizokuwa na kipashio chagizo ambazo zilidondolewa na
kuchanganuliwa kwa misingi ya nadharia tofauti. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo na
kupitia kwa vielelezo tungo.llibainika kuwa kipashio chagizo ambacho ni cha ziada katika virai
na vishazi vya Kiswahili sanifu huwa na miundo tofauti iliyoundwa kwa viambajengo tofauti na
kwamba chagizo hizi huwakilisha majukumu tofauti ya theta kutegemea kinafafanua kirai kipi
katika sentensi. Vilevile ilikuwa wazi kuwa chagizo zilizo na muundo sawia zaweza kuwakilisha
majukumu tofauti ya theta kulingana na kitenzi kinachotoa jukumu hili la theta kwacho.
v
Publisher
University of Nairobi
Subject
Muundo Na Uamilifu Wa ChagizoRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [605]
The following license files are associated with this item: