Lugha Katika Idara Ya Uhamiaji Nchini Kenya:mfano Wa Idara Ya Uhamiaji Mombasa
View/ Open
Date
2017Author
Otuchi, Timothy M
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu ulihusu uchunguzi wa lugha yamazungumzo katika Jdara ya Uhamiaji nchini Kenya.
Ni utafiti uliokuwa na malengo mawili ambayo ni; kubainisha aina za sentensi zinazotumika
katika mazungumzo katika Jdara ya Uhamiaji; na kubainisha uhamishaji na uchanganyaji
msimbo na sababu zake katika Idara ya Uhamiaji. Tulifanya hivi kwa kuzingatia aina na miundo
ya sentensi zinazotukia katika matumizi ya lugha baina ya wanaidara wenyewe na baina ya
wanaidara hao na wahudumiwa ambao ni jumla ya umma unaokuja kutafuta huduma katika ofisi
hizi. Ukiukaji wa kanuni za kisarufi ni wa hali ya juu, sentensi mseto hutumiwa kutegemea mada
ya mazungumzo japo nyingi ni sahili na viwango vya uhamishaji na uchanganyaji msimbo ni vya
juu vilevile. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili. Nadharia ya ujumlishaji usemi na ile ya
Bernstein ya msimbo pana na msimbo finyu. Nadharia hizi ziliteuliwa kutokana na ulinganifu
wake kwenye masuala yaliyochunguzwa katika utafiti. Utafiti huu ulibainisha kuwa Idara ya
Uhamiaji nchini Kenya husajili uhamishaji na uchanganyaji msimbo pamoja na miundo
mbalimbali ya sentensi. Lugha tatu kuu zinazohusika katika uchanganyaji na uhamishaji msimbo
ni Kiingereza, Kiswahili na lugha za kienyeji.
vii
Publisher
University of Nairobi
Subject
Lugha , Nchini KenyaRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [606]
The following license files are associated with this item: