Ukombozi wa kisiasa na kiuchumi katika mkamandume
View/ Open
Date
2015Author
Osango, Dinah S
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulikia suala la ukombozi wa kisiasa na kiuchumi katika Mkamandume ya S.
A. Mohamed. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchanganua hali ya kisiasa na kiuchumi katika
Visiwa vya Zanzibar na Pemba na kutathmini chanzo cha hali hiyo kwa kuihusisha na historia.
Aidha, tumechanganua mtazamo wa mwandishi kuhusu mambo yaliyopelekea mapinduzi ya
mwaka wa 1964 katika Visiwa vya Pemba na Zanzibar na athari zake kwa wananchi wa visiwa
hivi baada ya mkoloni kuondoka. Nadharia ambayo imetuongoza ni nadharia ya uhalisia wa
kijamaa ambayo ni ya kimapinduzi na inayosisitiza umuhimu wa kuielewa historia ya jamii
husika wakati wa kuhakiki kazi ya fasihi huku jamii husika ikisawiriwa kiyakinifu. Utafiti wetu
uligundua kuwa, matatizo yanayowakumba wananchi wa visiwa vya Zanzibar na Pemba yana
misingi yake katika historia ya jamii hii na kulingana na Mkamandume, hali ya kisiasa na
kiuchumi imeendelea kuwa mbaya zaidi baada ya mkoloni kuondoka kiasi cha kuwepo kwa haja
ya ukombozi wa pili.
Publisher
University of Nairobi
Subject
Ukombozi wa kisiasa na kiuchumiRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [625]
The following license files are associated with this item: