Mchangowa Vijana Kuleta Mabadiliko Chanya Katika Tamthilia Teule Za Kiswahili
View/ Open
Date
2012Author
Kiongera, Kiarie J
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Kazi hii inahusu juhudi za vijana kama mawakala wa mabadiliko chanya katika tamthilia nne
za Kiswahili. Tamthilia hizi ni Kifo Kisimani naMaua Kwenye Jua fa Asubuhi zilizoandikwa
na Kithaka wa Mberia . Pango na Seserumbe, zilizoandikwa na KW. Wamitila
Tumeongozwa na nadharia ya Ki-Foucault iliyoasisiwa na Micheal Foucault. Huyu ni
mwananadharia wa Kifaransa aliyeishi baina ya mwaka wa 1926 hadi 1984. Tunaangazia
mtazamo wake kuhusu mahusiano ya mamlaka na upinzani unaozuka pale panapokiukwa
maadili ya mahusiano yenyewe. Upinzani tunaouchanganua ni ule unaoongozwa na wahusika
vijana katika tamthilia nne tulizoziteua
Katika sura ya kwanza, tumechunguza maswala ya kimsingi yanayodhamiria kujenga msingi
wa utafiti wetu kama vile: Sababu za kushughulikia mada, tatizo la utafiti, yaliyoandikwa
kuhusu vijana, upeo na mipaka ya utafiti. Tumeongozwa na nadharia tete zifuatazo: kwamba
vijana wamefanikiwa kuyaleta mabadiliko na kwamba wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali katika jitihada zao.
Katika sura ya pili tumeijadili dhana ya vijana na kuyachunguza maovu ya kisiasa, kiuchumi
na kijarnii. Hapo tumewaonyesha vijana wakikabiliana na maovu hayo ili kuleta mabadiliko
chanya.
Katika sura ya tatu tumechunguza mafanikio waliyoyapata vijana katika kuzibadilisha jarnii
zao. Pia tumechunguza changamoto zinazowakabili katika harakati zao za kuleta mabadiliko
chanya
Katika sura ya nne tumetoa muhtasari wa utafiti rnzima na mapendekezo ya tafiti zaidi
zinazoweza kufanywa kuhusiana na mada yetu.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [606]
The following license files are associated with this item: