Uhakiki Wa Fani Katika Tenzi Za Howani Mwana Howani Na Mwanakukuwa Za Zaynab Himid Mohammed
Abstract
Utafiti huu unahusu uhakiki wa fani katika Tenzi za Howani Mwana Howani na
Mwanakukuwa zilizotungwa na Zaynab Himid Mohammed.
Kazi hii imegawika katika sura tano. Katika sura ya kwanza tumeelezea tatizo la utafiti,
sababu za kuchagua mada hii na kuorodhesha madhumuni ya utafiti huu. Isitoshe,
tumeufafanua msingi wa nadharia tuliotumia katika utafiti huu na kupitia yaliyoandikwa
kuhusu mada tunayoishughulikia. Katika sura ya pili tumeeleza dhana ya fani hatimaye
tumetaja na kufafanua kwa kina vipengele mbalimbali vya fani. Vipengele vya fani
tulivyoshughulikia ni wahusika, mandhari, toni, wakati, usimulizi, msuko, umbo na
lugha. Tumeeleza maana zake na jinsi vinavyotumika katika uhakiki wa kifani. Katika
sura za tatu na nne tumezihakiki tenzi za Howana Mwana Howani na Mwanakukuwa
kwa kutumia misingi ya uhakiki wa kifani kama tulivyofafanua katika sura ya pili.
Tumetathmini jinsi msanii alivyotumia vipengele vya fani kujenga kazi zake. Kwa kila
kipengele tumetoa mifano kutoka katika tenzi kuonyesha namna fani hizo zilivyojenga
tenzi. Sura ya tano ni hitimisho ambapo tumeeleza tuliyoyatambua na kutoa
mapendekezo ya utafiti zaidi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: