Uchanganuzi wa kiisimu wa baadhi ya semi katika matini ya kidini: mtazamo wa kipragmatiki
View/ Open
Date
2015Author
Shaviya, Lydiah M
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Lengo kuu katika utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza matumizi ya lugha katika mahubiri ya
kidini ya Kiswahili. Tasnifu hii inahusu uchanganuzi wa kiisimu wa baadhi ya semi katika
mahubiri ya kidini ya Kiswahili katika mtazamo wa kipragmatiki. Katika utafiti huu tulijikita
katika mahubiri ya kipentekoste tuliyorekodi kutoka katika vituo vya runinga vitatu teule
ambavyo ni KBC, SAYARE na MBCI. Tuliongozwa na nadharia ya pragmatiki leksika ambayo
inachunguza jinsi maana ya neno kiisimu inabadilika katika matumizi. Utafiti huu ulidhihirisha
ya kuwa wahubiri wa kidini hutumia baadhi ya semi zenye maana ya kiisimu ni tofauti na maana
ya kimuktadha japo kwa viwango tofauti. Vilevile, muktadha wa matumizi ya baadhi ya semi
katika mahubiri ya kidini ya Kiswahili huathiri maana katika kiwango cha matumizi ya elementi
za kiisimu. Pia ilidhihirika kuwa matumizi ya baadhi ya semi katika mahubiri ya kidini
kipragmatiki yana umuhimu.
Publisher
University of Nairobi
Collections
- Faculty of Education (FEd) [6020]